TANZANIA itacheza na Uganda mchezo maalum wa kirafiki

TANZANIA itacheza na Uganda mchezo maalum wa kirafiki kujipima nguvu kabla ya kucheza na Msumbiji kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika 2015.
BIN ZUBEIRY inafahamu Mashirikisho ya Soka Uganda (FIFA) na Tanzania (TFF) tayari yamefikia makubaliano juu ya mchezo huo ambao utachezwa Dar es Salaam katika tarehe ambayo itatajwa hivi karibuni.
Wakati Tanzania itacheza na Msumbiji mwezi ujao, Uganda itamenyana na Equatorial Guinea kusaka nafasi ya kuingia kwenye makundi baada ya kuitoa Madagascar.6670857301049624002

Taifa Stars itacheza mechi yake kwanza na Mambas Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Julai 19 na 20 mwaka huu, wakati mechi ya marudiano itafanyika Msumbiji kati ya Agosti 2 na 3 mwaka huu.
Stars ambayo iiliitupa Zimbabwe ‘Mighty Warriors’ kwa jumla ya mabao 3-2, ikitoa sare ya 2-2 baada ya kushinda 1-0, inatarajiwa kuingia kambini Juni 11, kuanza maandalizi.
Mechi nyingine za hatua hiyo ya mwisho ya mchujo zitakuwa kati ya Lesotho na Kenya, Kongo na Rwanda, Botswana na Guinea Bissau, Sierra Leone na Shelisheli na Benin na Malawi.

Advertisements
By ramadhaniabubakari